Sababu tatu za Waziri wa Mazingira, January Makamba kuivunja bodi ya NEMC

645
0
Share:

Waziri wa Ofisi Makamu wa Rais anyeshughulikia Mazingira na Muungano, January Makamba jumatatu ya Julai 17, 2017 ametangaza kuivunja bodi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Waziri Makamba amesema sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kushindwa kufikia malengo aliyojiwekea ambapo amebaini NEMC kuwa na mapungufu makubwa matatu ambayo ni rushwa, lugha mbovu na ucheleweshaji kibali cha ukaguzi.

“Sababu za mabadiliko ya Bodi ya NEMC ni ucheleweshwaji wa vibali vya ukaguzi wa mazingira na tuhuma za rushwa kwenye usimamizi sasa kutokana na mapungufu makubwa ndani ya NEMC, tumeamua kuivunja bodi hii kuanzia leo na viongozi wengine tutawatangaza leo,” amesema Makamba.

“Wapo pia baadhi ya watendaji wa NEMC tuliowasimamisha kazi ili ufanywe uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kabla kuchukua hatua … wote tuliowachukulia hatua leo uchunguzi wa awali ulitosheleza kuwachukulia hatua stahiki, hatua nyingine zitafuata baadaye.”

Aidha Waziri Makamba alizungumza kuhusu mwenyekiti wa bodi ya NEMC kama na yeye kwa bodi hiyo kufutwa uteuzi wake utakuwa umetenguliwa au ataendelea na kusema, “Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC ambaye uteuzi wake hufanywa na Rais ataendelea kuwepo hadi utakapofanyika uteuzi mwingine.”

Share:

Leave a reply