Saint Gobain yatoa mafunzo kwa wadau wa Ujenzi Tanzania

111
0
Share:

Kampuni ya Imports International Tanzania ambayo ni waagizaji na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi leo iliendesha warsha ya mafunzo juu ya matumizi ya vifaa vya drywall gypsum partition and pro-plaster wall finish ambavyo ni kwa ajili ya kumalizia ukuta kutoka Saint Gobain ambao ndiyo watengenezaji wa vifaa hivyo mafunzo yalifanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano mfupi wa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji, Trushal Jethwa alisema lengo la mafunzo lilikuwa ni kuwaleta pamoja makandarasi, wasambazaji na wafanyabiashara ili kuwajulisha  kuhusu maendeleo ya hivi karibuni katika sekta ya ujenzi ambayo ina ushindani mkubwa sana.

“Katika ulimwengu ambao teknolojia inabadilika haraka sana katika sekta ya ujenzi daima ni muhimu kuwapa wadau baadhi ya maendeleo ya hivi karibuni ili tuweze kukua pamoja kama timu, haisaidii sisi kuendelea kuwa na ujuzi huu bila wajulisha wadau wetu,” alisema Jethwa.

Mafunzo hayo yalitolewa na Saint Gobain ambao ni wazalishaji wa gyproc ambao wanaamini kuwa aina hii ya mafunzo inasisitiza ahadi yao ya kujenga uhusiano mzuri na jamii iliyowazunguka kwa ujumla.

“Hapa leo Saint-Gobain wanatueleza jinsi vifaa vyao vinavyochangia maisha ya kila siku, kwa kupitia bidhaa zake, wanaonesha utaalamu wa vifaa, utamaduni wa ubunifu, ufahamu wa mahitaji ya wateja na mbinu kwa njia ya uwazi na wajibu,” alisema Trushal Jethwa na kuongeza.

“Bidhaa za leo zinaonyesha thamani tunayowaletea wateja. Ninataka kila mtu ajue mambo muhimu ambayo Saint-Gobain inasimamia pamoja na nafasi za bidhaa zetu katika maisha ya kila siku.”

 Mtaalamu wa ujenzi kutoka Afrika Kusini, Member Mashabela akitoa elimu kuhusu ujenzi.

 Mtaalamu wa ujenzi wa kampuni ya Imports International Tanzania, Stanley Katabarwa akitoa melekezo wa washiriki wa mafunzo hayo.

Share:

Leave a reply