Sakata kuvuliwa uanachama wabunge CUF lamfikia Ndugai, kutoa maamuzi baadae

693
0
Share:
Job Ndugai

Spika Job Ndugai amepokea barua ya Profesa Ibrahim Lipumba, iliyomuarifu kuhusu uamuzi wa Baraza Kuu la CUF, kuwafukuza wabunge nane na madiwani wawili wa chama hicho, kwa makosa ya kinidhamu. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Ofisi ya Spika leo Julai 25, 2017 inaeleza kuwa, barua hiyo kutoka kwa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imeainisha makosa yapatayo sita ambayo yanakiuka kifungu cha 83(4) na (5) cha katiba ya CUF.

Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na Kukihujumu chama hicho katika uchaguzi wa marudio wa madiwani wa Januari 22  mwaka huu, Kumkashifu Mwenyekiti wa Taifa wa CUF Prof. Lipumba na Naibu Katibu Mkuu wake Magdalena Sakaya, kushirikiana na Chadema kupanga operesheni yenye lengo la kumuondoa mwenyekiti huyo madarakani, pamoja na kulipia pango na kufungua ofisi ya CUF magomeni bila kufuata taratibu za kikatiba.

Kufuatia makosa hayo, taarifa hiyo inaeleza kuwa, “Spika angependa kuuarifu umma kuwa, suala la kuwaondoa uanachama ni la utashi wa vyama vyenyewe na kila chama kina utaratibu wake. Hivyo bado anaendelea kuitafakari barua hiyo na taarifa rasmi kuhusu maamuzi ya spika kwa wabunge waliofukuzwa ataitoa hapo baadae.”

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply