Sakata la askari mgambo kutoa taarifa za uongo,lazua taharuki kubwa kwa ndugu

295
0
Share:

Mkuu wa mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe, amekutana na wanahabari kuelezea tukio la juu ya taarifa zilizozangaa mjini Singida, kwamba Rahel Erasto (28) aliyefariki muda mfupi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji, kafufuka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa.

Mhandisi Mtigumwe  alisema kuanzia mapema asubuhi mwili huo ulikuwa ukifanyiwa uchunguzi wa kina na kundi la wataalam wa afya likiongozwa na Daktari bingwa kutoka Makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Dk. Ahmed Mataka.

img_9049Kaimu mganga mkuu mkoa wa Singida,Dk.Ramadhan Kabala,akitoa taarifa juu ya maiti kufufuka ikiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini hapa.

img_9064Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,SSP Mayala Towo,akitoa taarifa juu ya kushikiliwa kwa mwajiriwa wa hospitali ya mkoa mgambo Emmanuel Daghau (28) kwa tuhuma ya kutoa taarifa za uongo kwa ndugu wa marehemu Rahel na jeshi la polisi juu ya kufufuka kwa maiti akiwa chumba cha kuhifadhia maiti.

img_9091Baadhi ya waombolezaji wa msiba wa Rahel Erasto aliyefariki dunia na kudaiwa kufufuka.Rahel alifariki dunia muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya mtoto kutolewa tumboni.

img_9076Mkuu wa mkoa wa Singida,mhandisi Mathew Mtigumwe,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  juu ya taarifa zilizozangaa mjini Singida,kwamba Rahel Erasto (28) aliyefariki muda mfupi baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji,kafufuka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mkoa.

(Picha zote na Nathaniel Limu).

Share:

Leave a reply