Sanamu la Lionel Messi lavunjika

952
0
Share:

Sanamu la staa wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi limekutwa limevunjwa na watu wasiojulikana likiwa limebakia na sehemu ya chini ya kiuno huku sehemu ya juu ikiwa haipo.

 

Sanamu hilo lililopo mji wa Buenos Aires, Argentina lilijengwa kwa ajili ya kumshawishi Messi kurejea katika timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu limekutwa likiwa nusu na mhusika wa tukio la kuvunja sanamu akiwa bado hajajulikana.

 

Aidha taarifa ambayo imetolewa Serikali ya jiji la Buenos Aires imesema kuwa tayari wameanza kufanya maandalizi ili kulijenga tena na kurejea kuwa kama awali.

 

“Kitendo ambacho kimefanyika ni uharibifu wa sanamu la Lionel Messi ambao umeacha sanamu bila kuwa na sehemu ya juu. Marekebisho tayari yanaanza kufanyika,” ilisema taarifa hiyo.

Share:

Leave a reply