Sauti za Busara 2017,watoa kipaumbe kwa vikundi vya muziki wa Reggae

659
0
Share:

Ushiriki wa Wasanii watatu wa muziki aina ya Reggae na bendi zao kwenye  tamasha la 14 la Sauti za Busara  lenye kauli mbiu #AfricaUnited unaashiria kuwa ni wakati muafaka kwa wadau wa muziki Tanzania kuutazama muziki wa Reggae kwa jicho la pili.

Kupitia jukwaa la Sauti za Busara  muziki wa Reggae umepewa uzito mkubwa kwa kuwa hubeba ujumbe mzito wa umoja, amani, upendo pamoja na kuibua mabaya yote yanayoendelea kwa jamii husika.

Kupitia nafasi hizo tatu zilizotolewa na uongozi wa Sauti za Busara ni changamoto kwa wanamuziki chipukizi na mameneja wa muziki kuwekeza kwenye muziki wa Reggae Tanzania kama ilivyo kwa aina nyingine ya muziki.

Vikundi hivi  ni miongoni mwa vikundi 40 vya muziki vitakavyotumbuiza ni pamoja na Rocky Dawuni kutoka Ghana, Sami Dan na Zewd band kutoka Ethiopia na Bob Magharib kutoka Morocco.

Mkurugenzi wa tamasha Yusuf Mahmoud amesema, “wasanii hawa watatu wa Reggae wanawakilisha vema muziki wa Reggae kwa  bara la Afrika. Tuna hakika kuwa Watanzania wengi wanapenda Reggae  si kwa midundo yake tu bali ni pamoja na ujumbe wa matumaini kwa wote wanaopigania haki na uhuru,”.

Bob Maghrib ni kundi lililozinduliwa mwaka 2011 lenye muunganiko wa wanamuziki wanaowakilisha tasnia ya muziki Morocco.  Kundi hili pia linamuenzi mwanamuziki maarufu wa Reggae  Bob Marley.

Sami Dan ana taaluma ya uhandisi  mwenye  shauku na muziki.  Harakati zake za kimuziki  zilianza kwa kuandika nyimbo na kufanya kazi kwenye bendi  akiwa kidato cha tano na sita.

Mwaka  2014, Sami Dan aliunda bendi ya  Zewd  nyimbo zake kama ‘Fikir Selam’ au ‘Love, Peace’  huburudisha mashabiki wake  kwa ujumbe wa amani na umoja.

Tamasha la  Sauti za Busara lilitajwa na CNN kuwa ni kati ya matamasha 7 ya muziki  Afrika ya kutazamwa litafanyika tarehe 9-12 February Ngome Kongwe Zanzibar.

Kundi la Bob Magharib kutoka Morocco.

Rocky Dawuni kutoka Ghana

Sami Dan na Zewd band kutoka Ethiopia

Mkurugenzi wa tamasha Yusuf Mahmoud akionesha kitabu chenye programu za tamasha hilo kwa wanahabari Jijini Dar es Salaam (Hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara, Mh. Simai Mohamed Said na kushoto ni Meneja wa Tamasha la Sauti za Busara, Journey Ramadhan.

Share:

Leave a reply