Semina ya kuwanoa Wadau wa Sekta ya Sanaa, yafanyika jijini Dar es Salaam

373
0
Share:

Kwa mara ya kwanza, wadau wa Sanaa nchini wamepata fursa ya kukutana na Makampuni, Mashirika na Vyombo mbalimbali katika mafunzo yaliyofanyika hotel ya Hyatt Regency,jijini Dar es Salaam. Semina hii iliongozwa na Maria Sarungi Tsehai, ambaye ni mdau mkubwa katika sekta hii

Mafunzo hayo yalifanywa na wataalam kutoka sekta mbalimbali kama Nyumba, Urembo, Saikolojia, Sanaa na Wasanii n.k.

c13

Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba (NHC), Arden Kitomari,akitoa mafunzo ya namna ya kuwekeza katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania,hususan kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa.

c16

Wadau wa Sanaa pia walipata mafuzo ya Namna ya kubalansi maisha yao ya Sanaa na yale ya Familia, kutoka kwa mwanasaikolojia maarufu, Aunt Sadaka Gandi.

c12

Semina hii iliyopewa jina Celebrity Corporate Conference & Cocktail iliwahusisha pia COSOTA na BASATA ambao ni wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa na taratibu zake.

c21

Bi. Doreen Anthony Sinare, CEO wa COSOTA akitoa somo kuhusu usajili wa kazi, masharti ya kuzingatiwa na Sheria zinazomlinda Msanii aliyesajiliwa.

c18

Sekta lengwa katika semina hii ni wadau kutoka Filamu, Muziki, Urembo, Habari, na Wajasiriamali mashuhuri.

c22

Bwana Aristides kutoka BASATA aliwaelekeza wadau kuhusu Taratibu mpya za kujisajili na chombo hiki, pamoja na faida zake.

c25

c23

Je, Unafahamu namna ya kuifanya Talanta yako kuwa Biashara? Hii ndio ilikuwa mada iliyoongozwa na Mjasiriamali mashuhuri, Shekha Nasser wa Shear Illusions.

c24

Baada ya mada zote kukamilika, wadau walipata fursa ya kubadilishana mawazo na kujadili walichojifunza, kwa kushiriki Tafrija mchapalo iliyoandaliwa.

Jokate Mwegelo

Huu ukawa wakati muafaka wa wasanii kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao kwa Makampuni, Mashirika na vyombo vinavyohusika na Sanaa na Wasanii. Mrembo na Mjasiriamali Jokate Mwegelo akiteta jambo na Afisa kutoka BASATA.

c29

Mwanahabari Maimuna Kubegeya hakuwa nyuma kuuliza maswali na kufahamiana na CEO wa COSOTA, Bi. Doreen Anthony Sinare.

c36

MwanaBlog maarufu John Bukuku akifurahia jambo na Meneja Masoko wa NHC, Arden Kitomari.

c41

c37

Antu Mandoza akisisitiza jambo.

c42

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Popular Links ambao ndio waandaaji wa Semina hii akiwa katika pozi na Mkurugenzi Ruge Mutahaba kutoka Clouds Media.

c43

Warembo katika picha ya pamoja.

c

Wasanii wa kutengeneza muonekano kutoka LuvTouch Manjano ya Shear Illusions, wakiwaonesha baadhi ya wageni, namna ya kupaka makeup.

c27

Mariam Ndabagenga, Mkurugenzi wa Popular Links akitoa neno la Shukran kwa wageni waalikwa wote na kuwakaribisha kwenye awamu ya pili ya Semina hii itakayofanyika mwezi Oktoba.

Semina hii ya Celebrity Corporate Conference & Cocktail imeandaliwa na Kampuni ya Popular Links kwa udhamini wa Heineken, The Guardian, Nipashe, Leteraha, Hyatt Regency hotel, Ndovu Special Malt, Cocacola, NHC, COSOTA, Jamii Media, BASATA, Shear Illusions, Clouds Media na Slide Visuals.

 

Share:

Leave a reply