Serena Williams ameshinda Wimbledon na kutengeneza rekodi mbili mpya, zipo hapa

250
0
Share:

Fainali ya mashindano ya tenesi ya Wimbledon kwa upande wa anawake imamalizika kwa Mmarekani, Serena Williams kuibuka mshindi baada ya kumfunga Mjerumani, Anelique Kerber.

Serena amefanikiwa kushinda taji hilo kwa kumfunga Angelique seti 7-5 na 6-3, ushindi ambao umemfanya kuendelea kujiwekea historia katika mashindano makubwa ya tenesi ambayo amekuwa akishiriki.

Baada ya kushinda taji hilo, sasa ameweka historia mpya baada ya kufikisha mataji saba ya Wimbledon lakini kama hilo halitoshi amevunja rekodi ya Steffi Graf ya kushinda mataji makubwa ‘Grand Slam’ baada ya kufikisha idadi aliyokuwa nayo mchezaji tenesi huyo ya kuwa na mataji 22.

Pamoja na kuweka rekodi hizo mbili ambazo hazikuwepo awali lakini unapaswa kufahamu kuwa Serena Williams ndiyo anaongoza katika orodha ya wachezaji bora wa tenesi kwa upande wa wanawake.

Share:

Leave a reply