Serikali kufanya marekebisho ya sheria zinazoibana tasnia ya sanaa

464
0
Share:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema wizara yake inapitia upya sheria zenye mapungufu zinazo gandamiza sekta zilizochini ya wizara yake ili katika kipindi cha Bunge la Bajeti zifanyiwe marekebisho.

Nape ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuwaaga wasanii wa WCB wakiongozwa na Nasib Abdul ‘Diamond’ wanaokwenda nchini Gabon kutumbuiza katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

“Wizara inapitia upya sheria zinazosimamia sekta zilizo chini ya wizara hii iili ziweze kuwa rafiki kwa wawekezaji hasa katika tasnia ya sanaa ili izidi kukua,” amesema.

Hata hivyo, Nape amesema tasnia ya sanaa inazidi kukua na kuitangaza nchi kimataifa.

“Sanaa yetu inazidi kukua na ndiyo maana wasanii wetu wanapata nafasi za kutumbuiza katika mashindano makubwa ,” amesema.

Share:

Leave a reply