Serikali ya Denmark yaikabidhi taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TaSUBa) vifaa vya kufundishia muziki

659
0
Share:

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao ameishukuru Serikari ya Denmark kwa kuwezesha kupatikana kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia Muziki kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)iliyopo Bagamoyo Mkoani Pwani.

Bi Milao alitoa shukrani hizo mapema jana Aprili 20.2017, wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ukumbi wa maonyesho wa TaSUBa, ambapo Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen alikabidhi vifaa vya kufundishia kwa awamu ya pili ambavyo ni kompyuta pamoja na vifaa vya kuhifadhia vyombo vya Muziki, vilivyotolewa na serikali ya Denmark.

“TaSUBa ni kituo chenye ubora uliotukuka Afrika Mashariki,inatoa mafunzo kwa watu kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki,ikipungukiwa na vifaa vya kufundishia ina maana hata kiwango cha mafunzo utapungua,hivyo ninaishukuru sana serikali ya Denmark kwa kutoa vifaa vya kufundishia hii itaifanya taSUBa kuendelea kutoa mafunzo bora na kuendelea kuwa kituo chenye ubora uliotukuka”alisema Bibi. Millao

Nae Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye alisema kuwa ,shughuli kuu ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo(TaSUBa) ni kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwenye Tasnia ya sanaa na utamaduni,utoaji wa mafunzo unakwenda sambamba na uwepo wa vifaa na miundombinu bora ya kutolea mafunzo hayo hivyo basi vifaa hivi vitasaidia sana uboreshaji wa mafunzo ya muziki yanayotolewa na TaSUBa .

Kwa upande wake, Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen Alisema kuwa Serikali ya Denmark inathamini sana masuala ya Sanaa na Utamaduni kwani kupitia Sanaa na Utamaduni mtu anaweza kutoa mawazo na maoni mbalimbali.

Katika awamu ya kwanza serikali ya Denmark kupitia kituo chake cha utamaduni CKU)iliipatia taasisi ya sanaa na utamaduni bagamoyo vifaa vya kujifunzia muziki vyenye thamani ya shilingi milioni themanini (80),wakati katika awamu ya pili Denmark imetoa kompyuta pamoja makabati ya kuhifadhia vifaa vya muziki,katika awamu zote mbili serikali ya Denmark imeipatia tasuba jumla ya vifaa vyenye dhamani ya shilingi milioni mia moja.

Hafla hiyo iliambatana na onyesho fupi la Muziki wa asili lililofanywa na wakufunzi wa TaSUBa pamoja na Wanachuo.

Baadhi ya wanafunzi na walimu wa TaSUBa wakimpokea Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen wakati akiwasili katika Chuo hicho cha Sanaa Bagamoyo

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akipokelewa na wenyeji wakeNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye (kulia)

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akipata maelezo ya Taasisi hiyo kutoka kwa wenyeji wakeNaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye (kulia)

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akifurahia ngoma na matarumbeta ya chuo hicho sambamba na wenyeji wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  (kulia) na Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye (kushoto)

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akioneshwa  baadhi ya maeneo ya Taasisi hiyo na  Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akiangalia picha maalum zinachochorwa katika taasisi hiyo

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akioneshwa baadhi ya vifaa katika chumba maalum cha ala za muziki cha taasisi hiyo

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akiwa na wenyeji wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  (kulia) na Mtendaji Mkuu wa TaSUBa Dkt Herbert Makoye (kushoto) wakati wa zoezi hilo la kukabidhi vifaa vya muziki

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akikata utepe pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  (kushoto)

Balozi wa Denmark Mh. Einar Herbogard Jensen akipokea picha kama zawadi kutoka taasisi ya Sanaa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa Na Michezo ,Bibi Nuru Millao  

Baadhi ya wanafunzi na walimu wakipata picha ya ukumbusho na Balozi huyo 

Share:

Leave a reply