Serikali ya Somalia yajipanga kuwamaliza Al Shabaab

612
0
Share:

Baada ya kusababisha machafuko maeneo mbalimbali ya nchi ya Somalia, serikali ya nchi hiyo imesema kwa sasa imejipanga kuhakikisha inawamaliza wapiganaji wote wa kikundi cha Kiislamu cha Al Shabaab.

Hayo yamesemwa na Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed wakati akizungumza kwenye mkutano wa Somalia unaofanyika London, Uingereza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali duniani waishio nchini Uingereza na kutumia nafasi hiyo kueleza jinsi serikali yake imevyojipanga kupambana na Al Shabaab.

Mohamed alisema licha ya mipango iliyopo lakini ni muhimu serikali kuhakikisha inakuwa na silaha nzito ambazo zitawezesha kuwamaliza wapinzani wao na silaha hizo lazima ziwe na nguvu kuliko zinazotumiwa na Al Shabaab.

“Kwa muda mrefu majeshi yetu na makundi ya kigaidi wamekuwa wakipambana kwa kutumia silaha ya aina moja na zaidi AK47. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwekewa vikwazo ambavyo vinatunyima uwezo wa kutengeneza silaha nzito,

“Muda unakuja sasa Somalia kuwa na uwezo wa kuwa na silaha bora kuliko za magaidi,” alisema Mohamed

Share:

Leave a reply