Serikali yamtangaza Hassan Abbas kuwa mkurugenzi mpya wa idara ya habari-MAELEZO

241
0
Share:

Miezi mitano baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Assah Mwambene kuhamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, serikali kupitia wizara ya habari imemtangaza Hassan Abbas kuwa mkurugenzi mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtangaza, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema uteuzi wa Abbas umetumia kifungu cha Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002, kifungu namba 6(1)(b) ambacho kinatoa ruhusa kufanyika uteuzi baada ya aliyekuwa akisimamia nafasi kuondoka.

Aidha Nape aliwataka waandishi wa habari kumpa ushirikiano mkurugenzi huyo kwa kipindi chote ambacho atakuwa mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye pamoja na cheo hicho atakuwa na cheo kingine cha kuwa msemaji wa serikali.
“Napenda kumtangaza ndugu Hassan Abbas kuwa mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari-MAELEZO kuchukua nafasi ya Assah Mwambene aliyehamishiwa wizara nyingine lakini pia napenda kumshukuru Bi. Zamaradi Kawawa kwa muda wote ambao aliutumia kukaimu nafasi hiyo,” alisema Nape.

Hassan Abbas

Mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari-MAELEZO, Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa na Assah Mwambene.

Kwa upande wa Hassan Abbas alisema kuwa amepokea nafasi hiyo na yupo tayari kuanza kazi lakini hata kuwa tayari kuzungumza mambo mengi kwa sasa kwani anahitaji muda kwa ajili ya kuweka mipango yake hivyo kuwaomba waandishi wa habari kuwa huru na kushirikiana nae kwani hata yeye ameshawahi kufanya kazi kama mwandishi wa habari.

“Nimeshaandika na kulipwa kwa habari, nimeshakuwa mwajiriwa, nimeshakuwa mhariri wa gazeti la Jumapili, nimeshakuwa mhariri msaidizi na nikawa tena mhariri mkuu kwahiyo mnaweza kuona ni jinsi gani nimekaa katika kazi kwa kipindi kisichopungua miaka tisa, niwaombe tushirikiane,” alisema Abbas.

Share:

Leave a reply