Serikali yapokea zana za kukusanya taarifa za watoto waishio katika mazingira hatarishi

76
0
Share:

Serikali imepokea zana za kukusanya na kutoa taarifa za watoto walio katika mazingira hatarishi kwa ajili ya wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii inayojumuisha kata, vijiji na mitaa.

Zana hizo zimekabidhiwa leo mjini Dodoma kwa Kamisha wa Maendeleo ya Jamii Dkt. Naftal Ng’ondi na Shirika la John Snow Inc(JSI) kushirikiana na MEASURE Evaluation na PACT Tanzania kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii(CHSSP) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani(USAID).

Wakati wa makabidhiano hayo Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa ni muhimu kupeana taarifa katika utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyopo ili kuwe na matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo hivyo zana hizo zitasaidia katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi.

Dkt. Naftali Ng’ondi ameongeza kuwa Serikali kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuhakikisha mtoto anayeishi katika mazingira hatarishi anapata huduma stahiki.

“ Zana hizi zitasadia wasimamizi wa mashauri ya watoto ngazi ya jamii katika kuwasaidia watoto waliopo katika mazingira hatarishi” alisema Dkt. Ng’ondi.

Nae Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la John Snow Inc (JSI) Dkt. Tulli Tuhuma amesema kuwa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii unaosimamia na JSI unalengo la kuimarisha mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii.

“Zana hizi tisa ni matokeo ya ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Misaada la Maendeleo la Watu wa Marekani USAID na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa UKIMWI na zitawasaidia wasimamizi wa mashauri ya watoto kuweka kumbukumbu na kufuatilia mashauri ya kiulinzi, ustawi wa jamii na afya katika halmashauri na kutoa huduma pamoja na rufaa kwa watoto walio katika mazingira hatarishi”alisema Dkt. Tulli.

 Aidha, Dkt. Tulli ameongeza kuwa awali kulikuwa na muingiliano wa katika utoaji wa huduma na kusababisha ugumu katika kufanya ufuatiliaji wa huduma na upatikanaji wa takwimu.

Na Beatrice Lyimo, MAELEZO- DODOMA

Share:

Leave a reply