Serikali yatakiwa kuboresha mabaraza ya ardhi ya kata

118
0
Share:

Serikali imetakiwa kuimarisha utendaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata ili kuboresha ufanisi wa mabaraza hayo katika kuwafikia wananchi.

Wito huo umetolewa leo Februari 13 jijini Dar es Salaam na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kupitia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Felista Mauya wakati akitoa tamko la kituo hicho kuhusu usimamishwaji wa mabaraza hayo.

Mauya amesema usimamishwaji wa mabaraza hayo ni kinyume na sheria,kutokana kwamba serikali ilitakiwa kuboresha utendaji kazi wake badala ya uamuzi huo, ambapo amekiri kwamba mabaraza ya ardhi kata yana mapungufu katika utendaji kazi wake.

Katika hatua nyingine, Mauya amesema LHRC inaitaka serikali kufuata taratibu za kisheria katika utatuzi wa kero za wananchi sambamba na kuboresha vyombo vya utoaji haki kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi kujifunza na kufuata mifumo sahihi ya utoaji haki kwa kutambua kwamba mahakama ndio muhimili wenye mamlaka juu ya utoaji haki kwa mujibu wa katiba.  

Share:

Leave a reply