Serikali yatakiwa kuyapa kipaumbele makundi maalumu katika utekelezaji wa bajeti zake

259
0
Share:

Wizara pamoja na wadau wa maendeleo nchini, wametakiwa kuzingatia ustawi wa makundi ya watu yaliyo pembezoni ikiwemo wanawake na walemavu katika utengaji wa bajeti zake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto Sihaba Nkinga wakati akizindua Mdahalo wa Ushiriki wa Makundi yaliyo pembezoni kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo Ummy Mwalimu.

Makundi hayo yaliyo pembezoni ni pamoja na Wanawake, walemavu, watoto, wakulima na wafugaji.

Nkinga amesema kuwa, wadau wa maendeleo pamoja na wizara ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, inabidi wayatumie makundi hayo hususani la wanawake kwa kuwa lina watu wengi.

“Asilimia ya wanawake nchini iko 52 na kwamba kundi hili ni kubwa tukiliwezesha turapiga hatua, wadau wa maendeleo wizara zinapopanga bajeti zake zizingatie ustawi wa wanawake sababu ukiwezesha wanawake ni sawa na kuwezesha jamii kwa ujumla,” amesema.

Hata hivyo Nkinga amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuwezesha makundi yote yaliyo pembezoni ikiwemo wanawake kiuchumi pamoja na kuwaunganisha na vyombo vya fedha.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye ni Mkurugenzi wa Maendeleo UNDP Amony Manyama amesema wadau wa mdahalo huo watajadili namna ya kutekeleza mpango wa maendeleo endelevu wa UN.

Share:

Leave a reply