Serikali yavitaka vyombo vya habari kuacha kuwahusisha Marais wastaafu na mchanga wa madini

570
0
Share:

Serikali ya Tanzania kupitia Waziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imevitaka vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuacha kuwatuhumu Marais wastaafu kwenye sakata la mchanga wa madini kwani majina yao hayajatajwa kwenye ripoti ambayo Rais Magufuli ameipokea.

Katika taarifa ambayo imetolewa na Waziri Mwakyembe imeeleza kuwa kuna baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wamekuwa wakituhumu Marais wastaafu bila kujua athari zake kiasiasa na kijamii.

Share:

Leave a reply