Shah Rukh Khan akamatwa kwenye kiwanja cha Ndege Marekani

248
0
Share:

Nyota wa filamu kutoka Bollywood, Shah Rukh Khan amezuiwa na maafisa usalama katika kiwanja cha ndege mjini Los Angeles na mara baada tu ya kutua jijini hapo akitokea nchini India.

Khan ambaye ni maarafu kwa kucheza katika filamu mbalimbali nchini India pamoja na zile alizoshirikishwa huko Hollywood na kwingineko amesikitishwa na kitendo cha Kukamatwa na mamlaka za Marekani katika uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo Los Angeles.

Shah Rukh Khan aliwahi kuwekwa chini ya ulinzi na pia kufikishwa mahabusu na maafisa usalama wa viwanja vya ndege vya nchini marekani hapo awali, ila taarifa zilizopo ni kuwa haijajulikana mpaka sasa ni nini kilichopelekea kuwekwa chini ya ulinzi na itakuwa kwa muda gani.

Balozi wa Marekani nchini India amewaomba msamaha kwa kukamatwa kwa Khan na amesema kuwa mamlaka zinafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha tukio hilo halitokei tena.

2009 alizuiliwa kwa muda wa saa mbili  katia uwanja wa ndege wa Newark na aliachiliwa baada ya ubalozi wa India kuingilia kati lakini pia Mwaka 2012 Khan aliwahi kukamatwa na kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa White Plains karibu na jiji la New York kwa takribani dakika 90 hadi pale alipolipia faini ya kosa alilolifanya.

Star huyo aliyewasili katika jiji la Los Angeles Ijumaa aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter “Ninaelewa kikamilifu jinsi hali ya usalama wa Marekani na dunia ulivyo, lakini kukamatwa kwenye idara ya uhamiaji ya Marekani kila wakati inaudhi sana.

Na Derick Highiness

Share:

Leave a reply