Sherehe ya Malia yamzuia Obama kuhudhuria mazishi ya Muhammad Ali

242
0
Share:

Ikulu ya Marekani imetoa taarifa kuhusu Rais Barack Obama kama ataweza kushirikia mazishi ya gwiji wa masumbwi duniani, Muhammad Ali anayetaraji kuzikwa Ijumaa ya Juni, 10 wiki moja baada ya kupoteza maisha Ijumaa iliyopita.

Taarifa ambayo imetolewa na ikulu hiyo imeeleza kuwa Obama hataweza kuhudhuria mazishi hayo kutokana na ratiba kuingiliana na sherehe za kumaliza shule kwa motto wa Obama, Malia.

Ikulu imeeleza kuwa siku ya Ijumaa, Obama pamoja na mke wake Michelle watakuwepo Washington DC kwa ajili ya sherehe ya binti yao hivyo hatakuwa na nafasi ya kuhudhuria mazishi hayo.

Wakati huo huo, msemaji wa familia ya Muhammad Ali, Bob Gunnell alisema kuwa Obama na Ali walikuwa wakiwasiliana mara kadhaa kwa njia ya simu.

Mazishi ya Muhammad Ali yatafanyika Ijumaa nyumbani kwao alipozaliwa 1942, eneo linalofahamika kwa jina la Louisville, Kentucky.

Share:

Leave a reply