Shindano la Insha msimu wa pili kufanyika tena Novemba 2016-Zanzibar

274
0
Share:

The voice of the voiceless  ambao ni waandaaji wa shindano la Insha Visiwani Zanziba lenye dhumuni la kuinua vipaji vya wanafunzi kwa njia ya mashindano hayo linatarajiwa kuwa la kitofauti ikiwemo msimu wa awamu ya pili hapo Mwezi wa Novemba mwaka huu ikiwemo idaidi ya washiriki na zawadi nono  kutolewa kwa washindi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi na Mwanzilishi  wa shindano hilo, Bwana Omary Mdogwa amebainisha kuwa, wamejiandaa kuhakikisha wanafikia malengo ya kuinua vipaji kwa watoto na vijana wa skuli za Visiwani humo huku akiwaomba wadhamini kuendelea kujitokeza kwa wingi kwani milango ipo wazi.

“Msimu wa pili wa shindano hili la Insha unatarajia kufanyika tena mwezi Novemba mwaka huu. Tunaendelea kuwapongeza wadau wetu wakiweo Zanzibar connection ( COMNET), Print plus , Tropical air Zanzibar, City delivery service na Double tree by Hilton na wengie wengi kwa hatua yao ya kujitokeza kudhamini katika msimu wa kwanza ulioisha hivi karibuni na sasa tunatarajia msimu mpya hapo baadae pia tunawakaribisha sana” alieleza Bwana Omary Mdogwa.

Aidha, amefafanua kuwa, hadi sasa hotel ya Double tree itaendelea kutudhamini ili kufanya mashindano Zaidi. Akifafanua hilo, Meneja wa hotel hiyo Bi Mary Njoroge amebainisha kuwa, udhamini wao huo ni moja ya kushukuru jamii.

“Kwetu sisi Double Tree by Hilton kudhamini katika mashindano kama haya ni njia ya kusema asante kwa jamii hasa wanafunzi hivyo tutaendelea kuwaunga mkono na pia wadhamini wengine wajitokeze katika kusaidia hili jambo jema” alieleza Meneja huyo, Bi. Mary Njoroge.

Shindano la Insha linajumuisha wanafunzi mbalimbali wa shule za Mjini Unguja. Kwa msimu wa shindano lililopita  wanafunzi  wa kidato cha tatu na cha nne walipata kushiriki shindano hilo huku jumla ya washiriki 120 katika hatua ya awali walipata kushiriki na kisha kuchujwa hadi hatua ya fainali na kisha kupatikana washindi.

Blog MediaWaandaaji wa shindano la Insha wakiwa katika picha ya pamoja..

Share:

Leave a reply