Shirika la Utangazaji TBC ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya Nchi”-Rioba

377
0
Share:

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania –TBC, Dkt. Ayub Rioba amesema TBC itaendelea kushirikiana na Mashirika megine ya Umma katika ushirikiano wa kimaendeleo kwani uwepo wake ni nyenzo muhimu sana kwa Maendeleo.

Dkt. Rioba ameyasema hayo juzi wakati wa mkutano wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili ya Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21), Unaofanyika Ikulu Jijini Dar e Salaam.

Akizungumza muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi wa mkutano huo, ambao umezinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliyemwakilisha Rais Magufuli, Dkt. Rioba amebainisha kuwa wao kama Shirika la Umma wameanza kutembelewa na Mashirika mbalimbali ya Umma katika namna ya kujitangaza pamoja na kufikisha ujumbe kwa Umma kwani Shirika hilo ni chombo cha umma kinachotoa taarifa.

“Shirika la Utangazaji ni nyenzo muhimu sana kwa maendeleo. Kwanza kwa sababu ni chombo cha umma cha taarifa. Chombo ambacho kinawapa wananchi taarifa, kinachosaidia wajumbe wa mashirika mbalimbali kuwafikia walengwa wao.

Chombo ambacho kinaonesha wananchi na wadau wengine  na nini kinafanyika katika nchi yetu na hatua gani zinachukuliwa na Serikali na wadau wengine katika kufikia tunakwenda kule mpango wa maendeleo ya miaka mitano tunayokusudia.

TBC inadhima kubwa ya kuwa kiunganishi cha kuunganisha wananchi, wadau wa maendeleo, mashirika ya Umma na Serikali” amesema

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania –TBC, Dkt. Ayub Rioba akizungumza muda mfupi wakati wa uzinduzi wa mkutano huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania –TBC, Dkt. Ayub Rioba (kulia) akiwa katika mkutano huo na viongozi wengine wa mashirika ya Umma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa amepiga picha ya pamoja na viongozi wakuu wa mashirika ya Umma muda mfupi baada ya kuzindua mkutano huo.

Share:

Leave a reply