Simba SC kukutana na Waandishi wa Habari kila Jumatatu mchana

552
0
Share:

Klabu ya Simba iinatarajia kuzungumza na waandishi kesho Jumatatu Septemba 18, utakaofanyika majira ya kuanzia Saa 6, mchana huku mambo mbalimbali yakitarajia kuzungumzwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo kwa vyombo vya habari na Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano, Haji S. Manara amewaomba wanahabari nchini wa michezo kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo.

“Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi mdogo wa klabu kuanzia majira ya saa 6 mchana,pamoja na mengine yatakayozungumzwa hiyo kesho, Septemba 18,mkutano huu ni muhimu sana kwako/kwenu kuhudhuria kwani kuna mengi ya umuhimu ya kuyatolea ufafanuzi na kuyaweka wazi kwa umma wa mashabiki na wanachama wetu kupikia kwenu wanahabari” alieleza Manara kwenye taarifa yake hiyo.

Manara ameongezea: “Tunasisitiza kuwahi,kwani mkutano huo utaanza katika muda uliotajwa hapo juu  na utazingatia muda. Pia klabu inapenda kutoa taarifa rasmi,kuwa kuanzia sasa kila siku ya Jumatatu tu tutakuwa na mkutano na Wanahabari, kuanzia majira ya saa 6 mchana kwenye ukumbi wa klabu” ilieleza taarifa hiyo.

Share:

Leave a reply