Simba Sc yaendeleza unyama kibabe, yaitandika Mwadui 3-0

363
0
Share:

Mabao mawili ya mchezaji mwenye ‘njaa’  Mohammed Ibrahim na lile la moja la mshambuliaji anayecheka na nyavu kila kukicha, Shiza Kichuya yametosha kabisa kuipa pointi tatu na mabao matatu klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sc ambao ni vinara wa  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika mchezo wao huo wa leo dhidi ya Mwadui FC mchezo uliochezwa katika  Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

Mabao: Simba imepata mabao yake yaliyofungwa katika dakika ya  32′ na 51 na mchezaji wake Mohammed Ibrahim ‘MO’ 
huku dakika ya 43′ Shiza Kichuya akiendelea kutupia. Hadi kipenga cha mwisho Simba SC imeweza kujipatia mabao hayo 3-0..

Kwa matokeo hayo ambayo Mwadui itajilaumu yenyewe kwa kukosa nafasi muhimu za kushinda lakini hali ilikuwa tofauti na Simba iliweza kutumia nafasi hiyo na kupata ushindi huo mzuri.

Kwa upande wake Kocha Mayanja amesema Simba Sc wamejitahidi na kikosi chake kimekosa mabao ya wazi na ataweza kuyafanyia kazi makosa hayo.

Kwa upande wake Kocha wa Mwadui amebainisha kuwa, kikosi chake kilizembea na wapinzani wake kupata ushindi huo.

14907560_663632607129091_3193250276123590692_n14907037_663634853795533_8300977663360840659_n

Share:

Leave a reply