Simba SC yamwondoa Mzee Kilomoni kwenye baraza la wadhamini

407
0
Share:

Kamati ya utendaji ya Simba imesimamisha uanachama wa Mzee Hamis Kilomoni na kumuondoa kwenye baraza la wadhamini wa klabu kwa kupeleka kesi katika mahakama.

Uamuzi huo umefanywa katika mkutano mkuu wa Simba ambao unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere na nafasi yake imechukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi.

Pia kamati ya utendaji ya Simba imepanga kumtumia barua Mzee Kilomoni ya kumtaka afute kesi mahakamani na la sivyo atafutwa uanachama moja kwa moja.

Aidha katika mkutano huo Prof. Juma Kapuya amepitishwa kuwa mdhamini wa klabu ya Simba na kuchukua nafasi ya Marehemu Ally Klaiyst Sykes

Share:

Leave a reply