Simba SC yavunja mkataba na kocha Joseph Omog

1552
0
Share:

Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.

Uamuzi huo umekuja kufuatia timu hiyo kutolewa kwenye Kombe la Shirikisho katika mchezo wake wa kwanza na timu ya Green Warriors inayoshiriki Ligi Daraja la Pili kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji Manara, imeeleza kuwa baada ya kuvunja mkataba na kocha Omog, kwa sasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Juma.

“Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho (Desemba 24, 2017) , na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara, ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo,

“Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.” alisema Haji Manara.

Share:

Leave a reply