Simba yaisogelea Yanga kileleni

800
0
Share:

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Maji Maji na Simba umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 3-0, mchezo ambao umepigwa katika Uwanja wa Maji Maji uliopo Songea.

Ushindi umepatikana kupitia kwa Ibrahim Ajib ambae alifungua mlango wa magoli katika dakika ya 19 ya mchezo huo na goli la pili likifungwa na Said Ndemla katika kipindi cha pili, dakika ya 63 na Laudit Mavugo akihitimisha katika dakika ya 88.

Ushindi ambao Simba imeupata umeiwezesha kuwasogelea wapinzani wao Yanga kwa kufikisha alama 48 huku watani wao wakiwa na alama 49 na hivyo kuwa na tofauti ya alama moja.

Ligi Kuu ya Vodacom itaendelea kesho jumapili kwa mchezo mmoja kati ya Azam FC na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Chamazi ulioko Mbande, mchezo unaotarajiwa kuanza saa 1:00 usiku.

Share:

Leave a reply