SMZ yailipa TANESCO Bilioni 10, Prof. Muhongo asema hawatakata umeme Zanzibar

639
0
Share:

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kuanza kukata umeme kwa wadaiwa sugu, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema hawataikatia umeme Zanzibar licha ya kuwa na deni kubwa.

Prof. Muhongo ameyasema hayo baada ya Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kufanya mazungumzo yaliyohudhuriwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Kahitwa Bishaija na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa TANESCO, Sadock Mugendi.

Share:

Leave a reply