“Sogezeni huduma za bima kwa wananchi”- Dkt. Kijaji

233
0
Share:

Makampuni ya bima nchini yametakiwa kusogeza hudama za bima ya Maisha kwa wanananchi ili kuchangia ukuajia wa uchumi wa nchi hususan katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji alipokuwa akifungua semina ya kimataifa ya Bima ya Maisha inayofanyika jijini Arusha.

Sekta ya bima nchini, kama ilivyo kwa mataifa mengine Afrika, inakumbwa na changamoto nyingi zikiwemo mwamko mdogo wa wananchi kununua bima, huduma kutofikia wananchi, na elimu ndogo ya masuala ya bima kuhusu bidhaa tofauti tofauti za bima.

“Tanzania tuna idadi ya watu takriba ni milioni hamsini, hili ni soko kubwa sana na fursa kwa makampuni ya bima kuwekeza, kwa maana hiyo mna deni la kuwafikia wananchi kwa kuwa na bidhaa za bima zenye ubunifu na zenye kutatua matatizo yao” amesema Dr. Kijaji.

Serikali imejidhatiti katika kuimarisha sekta ya bima kwa kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza soko la bima kwa kurejesha imani ya wananchi juu ya huduma za bima zinazotolewa na makampuni yaliyosajiliwa nchini.

“Hili litachangia katika kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania, kwani ni lazima kisheria makampuni ya bima nchini kuwaajiri wazawa na tayari serikali ina vyuo vinavyotoa taaluma hii ya bima. Hivyo nina uhakika kuwa nguvu kazi yenye uweledi wa masuala ya bima inapatikana nchini” amesema Dr. Kijaji.

Pia Dr. Kijaji ameitaka Mamlaka ya Bima nchi kupitia Kamishna wa Bima Nchini Dr. Baghayo Saqware kushirikiana na makampuni yenye usajili nchini kuhakikisha biashara ya bima inakuwa imara na yenye kunufaisha watanzania kwa sababu makampuni haya yanakusanya amana kutoka kwa watanzania.

Mkutano huo wenye dhima ya “Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Nini mchango wa bima ya maisha katika kuleta maendeleo endelevu” umewawezesha washiriki wote wa sekta ya bima kutoka Afrika na nje ya Afrika kujadili mada mbalimbali ili kuboresha soko la bima nchini na Afrika kwa ujumla.

Na Oyuke Phostine.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitete jambo na Kamishna wa Bima nchini Dkt. Baghayo Saqware katika mkutano wa kimataifa wa Bima ya Maisha uliofanyika jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa Bima ya Maisha uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Umoja wa Makampuni ya Bima nchini Bw. Sam Kamanga akitoa mada katika mkutano wa kimataifa wa Bima ya Maisha uliofanyika jijini Arusha.

Kamishna wa  Bima  nchini Dkt.  Baghayo Saqware akielezea hatua zinazochukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa  Bima  nchini (TIRA)  Katika kuboresha huduma za bima.

Baadhi ya watoa mada na washiriki wa mkutano huu wakiendelea kufuatilia mada zilinawasilishwa katika Semina ya kimataifa katika Bima ya Maisha uliofanyika jijini Arusha.

Share:

Leave a reply