VIDEO: Switzerland, Wales waanza kwa kishindo EURO 2016

270
0
Share:

Baada ya mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya EURO 2016 na wenyeji Ufaransa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhifi ya Romania, mchezo wa pili wa Kundi A umechezwa leo jioni na Switzerland kuibuka na ushindi wa gooli 1-0 dhidi ya Albania.

Goli pekee na la ushindi kwa Switzerland katika mchezo huo lilifungwa na Fabian Schaer katika dakika ya 5 ambalo lilidumu hadi mchezo unamalizika, hata hivyo Albania walimaliza mchezo huo wakiwa nusu baada ya mchezaji wake Lorik Cana kuonyeshwa kadi nyekundu.

Mchezo wa pili ulikuwa wa Kundi B kati ya Wales na Slovakia ambapo Wales waliibuka na ushindi wa goli 2-1.

Magoli ya Wales katika mchezo huo yalifungwa na Gareth Bale dk. 10 na Robson-Kane katika dk. 81 huku goli pekee la Slovakia likifungwa na Ondrrej Duda katika dk. 61.

Share:

Leave a reply