Taarifa ya Ikulu inayomhusu JPM kuhusishwa kuzuia mzigo wa Mama Salma Kikwete bandarini

2338
0
Share:

Katika siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imechapisha taarifa zinazomhusisha Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Mama Salma Kikwete na Taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwamba ameshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoiingiza nchini na hivyo kuwa hatarini kupigwa mnada.

Taarifa hizo zimemhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa anahusika kuzuia mizigo hiyo bandarini mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo sio kweli na ni uzushi, kwani Rais Magufuli hajawahi kuzuia wala kuagiza kuzuiwa kwa mizigo ya Mama Salma Kikwete.

Rais Magufuli amesikitishwa sana na uzushi huo unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake na amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake vizingatie weledi na kufuata sheria.

“Nimesikitishwa sana na uzushi unaofanywa dhidi ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete, tafadhali wale mnaotengeneza uzushi huu acheni mara moja na muacheni Rais Mstaafu Kikwete apumzike.

“Rais Mstaafu Kikwete amefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa hili, amestaafu anapumzika, narudia muacheni apumzike, Serikali haitaendelea kuvumilia uzushi na uchonganishi huu unaofanywa kwa makusudi ili kuwachafua viongozi wastaafu” ameonya Rais Magufuli.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam,Gerson Msigwa kwa taarifa yake aliyoituma mchana wa leo 4 Desemba kwa vyombo vya habari.

220e08fa-e534-4380-8dfa-efb12abcb506

Share:

Leave a reply