Taarifa ya Wizara ya Viwanda kuhusu akaunti ya Twitter ya Waziri Mwijage

2647
0
Share:

Wizara ya Viwanda, Biashara ya Uwekezaji imetoa taarifa kuhusu akaunti ya Twitter inayotumia jina la waziri wa wizara hiyo, Charles Mwijage kuwa sio yake na ujumbe ambao inaandika una lengo la kumchafua waziri huyo.

Taarifa hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu akanuti hiyo ya Twitter kuweka ujumbe ambao unaelezea kitendo alichokifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kwenda Clouds Media akiwa na askari wenye silaha za moto.

Ujumbe ambao uliandikwa kwenye akaunti hiyo ulisema, “Kilichotokea kwa Clouds Media ni kitendo cha kinyama na wala si uungwana kabisa tunajenga nchi ya viwanda na si ya kutishiana”

Waweza kusoma taarifa kamili ya Wizara ya Viwanda hapa chini.

Share:

Leave a reply