Taasisi na Mashirika yatakiwa kusonga mbele kasi ya utekelezaji wa agizo la Usafi wa mazingira

250
0
Share:

Wito umetolewa kwa jamii, Taasisi na wadau mbalimbali kutopunguza kasi
katika kutekeleza kwa vitendo agizo la kufanya usafi wa mazingira,
kupanda miti na kulinda vyanzo vya maji alilolitoa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Desemba  9 mwaka jana.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA) Bi.Mary
Ntikula kufuatia  watumishi wa Mamlaka hiyo na wale wa Shirika la Maji
Safi  na Maji Taka Dar esalaam (DAWASCO) kufanya Usafi na kukabidhi
msaada wa vitu mbalimbali hospitalini hapo amesema kuwa wao kama
DAWASA wamejiwekea utaratibu wa kufanya usafi katika maeneo
yanayowazunguka kila mwisho wa mwezi kuunga mkono agizo la Mhe.Rais la
kufanya usafi kila jumamosi mwisho ya kila mwezi.

Amesema katika kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo utaratibu wa
kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka yakiwemo ya Hospitali
ya Mwananyamala na maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya maji pamoja
na shughuli za upandaji wa miti kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

Ameeleza kuwa Jumamosi ya kwanza ya mwezi huu wao kama DAWASA wameona
ni vyema wakaitumia kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali ya
Mwanayamala kwa kutambua mchango wa hospitali hiyo katika kuhudumia
afya za wagonjwa wanaotoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
essalaam.

Ameongeza kuwa wao kama wafanyakazi wa DAWASA wameungana na wenzao wa
DAWASCO kufagia, kufyeka, kusafisha mifereji na kuondoa maji taka
katika hospitali hiyo pamoja na kutoa zawadi zinazoendana na usafi
zikiwemo maji, mafuta, sabuni za kuogea na kufulia pamoja na mafuta ya
kujipaka watoto wadodo na vitu mbalimbali kwa matumizi ya wagonjwa ili
kuonyesha upendo wao.

” Leo tumekuja hospitali ya Mwanayamala kufanya usafi na kutoa zawadi,
tumezunguka mazingira yote, tumefagia, tumefyeka, tumezoa uchafu na
pia kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa zinazohusiana na usafi na
nyingine tumewapatia viongozi wa hospitali ili waendelee kudumisha
usafi katika hospitali hii” Amesisitiza na kuongeza kwamba wao kama
DAWASA wataendelea kusaidia hospitali hiyo katika maeneo mbalimbali.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DAWASCO Mhandisi Shabani
Mkwanywe amesema wao kama DAWASCO wameitikia wito wa Mhe.Rais kwa wa
kufanya usafi kila jumamosi ya kwanza ya kila mwezi kwa kugawanyika
katika maeneo mbalimbali kufanya usafi ikiwemo hospitali ya Muhimbili.

Amesema wao wanafanya kazi na jamii na wataendelea kuwajibika kwa
jamii kwa kile wanachokipata na kutoa wito kwa Taasisi na mashirika
mengine kuitumia siku hii kufanya usafi ili kuepuka magonjwa ya
milipuko.

Aidha, amesema DAWASCO katika kutekeleza majukumu yao wataendelea
kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuondoa
changamoto iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa mkoa wa Dar es salaam na
wakazi wa Kibaha na Pwani mkoani Pwani ya uhaba wa maji kufuatia
uzalishaji wa maji ya kutosha uliopo sasa.

Naye Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari wa
watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa
mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo amewashukuru
watumishi wa DAWASA na DAWASCO kwa kujitoa na kufanya usafi.

Ameeleza kuwa hospitali hiyo licha ya kupata huduma ya uhakika ya maji
safi bado inakabiliwa na changamoto ya uondoaji wa majitaka kwenye
mashimo yaliyopo hospitalini hapo kutokana na mfumo wa uliopo
kutounganishwa kwenye mfumo mkuu unaopeleka maji taka baharini  jammbo
linaloifanya hospitali hiyo kujikuta ikitumia gharama kubwa kuondoa
maji hayo.

” Maji taka tunayozalisha kwa siku ni mengi sana, tunawashukuru DAWASA
na DAWASCO kujitolea kunyonya maji taka yote katika mashimo sasa
tutakaa miezi 6, ninyi wenyewe mtakua mashahidi gharama ya uondoaji wa
maji haya ni kubwa tumekuwa na kero ya vyoo kufurika na wakati
mwingine kuziba”

Aidha, amesema kuwa hospitali ianaendelea na mradi wa jengo la ghrofa
5 kwa lengo la kupunguza msongamano wa wagonjwa walioko kwenye wodi 11
ambazo zote zimejaa wagonjwa huku akibainisha kwamba hospitali hiyo
ina hudumia zaidi ya kniniki 11 pia wagonjwa 1500 hadi 2000 kwa siku.

Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi za
serikali katika kuboresha huduma za afya hospitalini hapo kama
walivyofanya DAWASA na DAWASCO.

Nao baadhi ya wagonjwa wa hospitali hiyo waliopata fursa ya kuzumza
mara baada ya kukabidhiwa misaada hiyo akiwemo Bi.Stella Mkufya
anayeuguza mwanae katika wodi ya watoto hospitalini hapo ameishukuru
DAWASA na DAWASCO kwa misaada waliyoitoa.

Amesema kuwa mbali na kupokea misaada ya vitu anafurahishwa na ubora
wa huduma zinazotolewa kutoka kwa madaktari wa hospitali hiyo na
kuiomba Serikali iendelee kuongeza majengo na vitanda vya wagonjwa
katika hospitali hiyo.

” Nawashukuru DAWASA na DAWASCO kwa msaada waliotupatia pia
nawashukuru madakatari wa hospitali hii kwa huduma nzuri
wanayotupatia, kwa kweli huduma ya hapa ni nzuri sana naiomba Serikali
ituongezee vitanda na magodoro” Amesema.

Na.Aron Msigwa-MAELEZO.

imageViongozi wa DAWASA wakishiriki katika zoezi  la usafi. Kutoka kushoto  ni Mary Ntukula, Mkurugenzi wa utawala na kulia ni Eng  Romanus  Mwang’ingo Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi.  Katikati ni Neli Msuya  Meneja mahusiano  ya jamii.

image_2Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakijiandaa kuingia kwenye
wodi za wagonjwa kugawa misaada ya vitu mbalimbali.

image_1Baaadhi ya watumishi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la usafi katika Hospitali ya Mwananyamala.

image_3 image_4Watumishi wa DAWASA na DAWASCO wakigawa msaada wa vitu
mbalimbali kwenye wodi za wagonjwa

image_5Kaimu mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye pia ni Daktari wa watoto, Delila Moshi akizungumza mara baada ya zoezi la usafi wa mazingira na ugawaji  wa misaada katika hospitali hiyo uliofanywana
watumishi wa DAWASA. Picha zote na Aron MSigwa- MAELEZO. .

Share:

Leave a reply