Taasisi ya Kilimo ya Agro For Help Foundation yazinduliwa rasmi nchini

746
0
Share:

Taasisi ya Kilimo ya Agro For Help Foundation ya Jijini Dar es Salaam inayojihusisha na masuala ya kunyanyua  na sekta hiyo ya Kilimo nchini leo 31 Januari 2017, imezinduliwa rasmi  mbele ya wadau wa Kilimo na viongozi wa Serikali tukio lililofanyika Jijini Dar e Salaam leo.

Awali katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda ambaye aliwakilishwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa  amewapongeza  Agro  For Help Foundation, kwa kuja na mpango wao huo  kwani ni miongoni mwa sekta zinazoinua uchumi wa Tanzania huku akiwataka zaidi kujikita katika kutoa elimu  ya Kilimo  na pia suala la  taarifa  kwa wakulima  juu ya Kilimo na Masoko.

Mgeni huyo rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi zilizoanzishwa kwa taasisi hiyo kwani zina manufaa kwa Watanzania na zitakuwa kimbilio kwa wakulima na wadau wa sekta hiyo Mama katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo ya Agro For Help Foundation, Bi. Mwaka Shukuru ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya Kilimo hapa nchini ikiwemo wadau binafsi wanaojihusisha na masuala hayo hivyo wanaamini watashirikiana na wadau wote ikiwemo Serikali katika kuendeleza kilimo na Wakulima kwa ujumla.

“Kupitia taasisi hii itasaidia kusambaza elimu ya kilimo cha biashara na kilimo cha kisasa. Tumebaini changamoto nyingi  ikiwemo mabadiliko ya tabiachi kwani  imekuwa nchangamoto hivyo  uwepo wetu tumeliona hilo na kikubwa ni kuona jinsi gani ya kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa elimu na kuhamasisha katika njia bora mbalimbali ikiwemo kilimo cha kisasa cha umwagiaji. Ameeleza Bi. Mwaka Shukuru.

Bi. Mwaka Shukuru ameongeza kuwa, mpaka sasa kufikia kuizindua rasmi imekuwapo zaidi ya mwaka  mmoja hapa nchini ambapo imejipanga sawasawa katika kusaidia wakulima  wadogo kwenda kwenye kilimo cha kati na kufanya kilimo ni biashara na kilimo ni ajira kwani wanaamini hii itapelekea kusaidia kukua kwa uchumi kupitia sekta hiyo ya kilimo na kupunguza umasikini huku kikitengeneza ajira kwa watanzania wengi zaidi.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa Kilimo hapa nchini anayejihusisha na kilimo cha matunda ikiwemo  cha Mapapai, Mwanadada Angella Kavishe amepongeza taasisi hiyo kwani anaamini itakuwa msaada zaidi kwa wakulima ambao mara zote wamekuwa wakijikita katika kilimo cha mazoea pekee ama kile cha kienyeji.

Tazama MO tv  hapa:

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akiwasili katika tukio hilo la uzinduzi wa taasisi ya kusaidia Kilimo nchini ya Agro For Help Foundation, tukio lililofanyika katika jengo la PSPF Makao makuu (Golden Jubilee Tower ).

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akitoa hutuba fupi wakati wa uzinduzi wa taasisi ya kilimo ya Agro For Help Foundation.

Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa taasisi ya Kilimo ya Agro Help Foundation

Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wadau wa kilimo wakati wa uzinduzi  rasmi wa taasisi ya Kilimo ya Agro  For Help Foundation.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi taasisi hiyo ya kilimo ya Agro For Help Foundation. Anayeshuhudia ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bi. Mwaka Shukuru

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi taasisi hiyo ya kilimo ya Agro For Help Foundation. Anayeshuhudia ni Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bi. Mwaka Shukuru.

Baadhi ya uongozi wa taasisi hiyo ya kilimo ya Agro For Help Foundation wakishuhudia uzinduzi huo pamoja na kupiga makofi mara baada ya Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa kukata utepe kuashiria kuzindua rasmi. Kushoto ni Mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Bi. Mwaka Shukuru, akifuatiwa na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi hiyo Bi. Neema Shukuru pamoja na Mtendaji Mwenza Bw. Robert Gunze

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akisalimiana na Mtendaji Mwenza Bw. Robert Gunze

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mh. Hashim Mgandilwa akifurahia jambo mara baada ya uzinduzi huo

Mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Bi. Mwaka Shukuru akuzungumza na waandishi wa habari

Mwanadada anayejishughulisha na kilimo cha matunda ikiwemo mapapai  Mkoani Kilimanjaro, Angella Kavisheakizungumza changamoto za kilimo na fursa za taasisi mpya ya Agro For Help Foundation itakavyosaidia kilimo hapa nchini

Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuzi  kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo wa PSPF, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS) kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kilimo waliofika katika shughuli ya uzinduzi wa taasisi ya Kilimo Agro For Help Foundation uliofanyika leo 31 Januaria 2017.

Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wadau wa kilimo wakati wa uzinduzi  rasmi wa taasisi ya Kilimo ya Agro  For Help Foundation. PSPF  ni miongoni mwa wadau waliojitokeza kudhamini tukio hilo la uzinduzi wa taasisi ya kilimo ya Agro For Help Foundation.

 

Share:

Leave a reply