TaESA yatangaza tarehe ya mwisho kupokea maombi ya kazi EACOP

202
0
Share:

Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) umetangaza tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya ajira katika mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi- EACOP.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mtendaji wa TaESA, Saneslaus Chandaruba amesema mwisho wa kupokea maombi hayo ni Machi 30 mwaka huu. 

Amesema, mradi huo unatarajia kuajiri zaidi ya watu 10,000 wakati wa utekelezaji ujenzi wa bomba na 1,000 wakati wa utekelezaji shughuli za mradi huo.   

 Chandaruba amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi hizo, huku akiwatoa wasi kwamba hakutakuwa na rushwa wala urasimu wa aina yoyote na kwamba watakaoajiriwa ni wale wenye sifa husika. 

Aidha, amesema watumaji wa maombi wanatakiwa kutuma maombi yao kwenye tovuti ya TaESA badala ya kupeleka barua katika ofisi za wilaya zao, kwani haitakuwa rahisi kwa wao kuzipata barua hizo.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply