Tajiri abadili fedha za harusi kujenga nyumba kwa ajili ya maskini

615
0
Share:

TAJIRI mmoja wa India kwa namna ya pekee alimua kusherehekea harusi ya binti yake kwa kuhakikisha anajenga makazi kwa ajili ya watu wasiokuwa na maeneo ya kuishi.

Kitendo hicho kimeelezwa na wachambuzi wa mambo kwamba kimeenda kinyume na tabia za kawaida za matajiri

Tajiri huyo Ajay Munot  ambaye ni mkazi wa Maharashtra amejenga nyumba 90 zenye thamani ya rupia milioni saba hadi nane sawa na dola za Marekani 103,000 hadi 118000.

Ujenzi huo uliwezeshwa na fedha zilizowekwa kibindoni kwa ajili ya kuwa na harusi ya kifahari ya binti yake.

Imeeelzwa na Indian Express kwamba mume na mke walikubaliana na wazo hilo. Mke aliona kwamba hiyo ni zawadi kubwa kwa sherehe yake ya harusi.

Nyumba hizo 90 zilijengwa katika eneo la mita za mraba 8,093 na gharama yake ikaongezeka na kufikia dola za Marekani 221,000. Nyumba zote hizo zitakuwa na maji ya kunywa ya bomba yaliyopitia mashine maalumu ya kuchuja. Aidha kila nyumba ipo katika futi za mraba 240 ikiwa na madirisha mawili na milango miwili.

Munot,ambaye anaendesha biashara ya jumla ya nguo na ngano alisema alitaka kuwasaidia watu maskini wanaoishi katika mazingira hatarishi wakiwa hawana nyumba ingawa walikuwa na tabia njema. yeye mwenyewe ndiye aliyechagua watu ambao watakuwa wanaishi katika nyumba hizo.

“Hii ni sura mpya katika historia na ni matumaini yangu kwamba matajiri wengine wataiga mfano huu,” alisema na kuongeza: “Tunawajibika katika jamii yetu na tunajitahidi  kutekeleza.”

Kwa utamaduni harusi za India zimetawaliwa na kupeana zawadi kubwa kubwa kuonesha utajiri lakini ni nadra sana kuona matumizi yenye maana kwa wasiokuwa nacho.

Share:

Leave a reply