Tamasha la Chakula la Mji Mkongwe kuanza Oktoba 9, hoteli na migahawa kushiriki

284
0
Share:

Tamasha la Chakula la Mji Mkongwe linatarajiwa kuanza Oktoba 9 ya mwaka huu na kumalizika Oktoba 14 ambapo litafanyika katika eneo la Mji Mkongwe visiwani Zanzibar na hoteli na migahawa mbalimbali inatarajiwa kushiriki.

Katika tamasha hilo ambalo li la pili kufanyika baada ya la mwaka jana 2016 watalii na wazawa kutoka maeneo mbalimbali wanatarajiwa kushiriki na vyakula vya mataifa mbalimbali vitakuwepo katika tamasha vikipikwa na wapishi kutoka sehemu mbalimbali ikiwepo hoteli ya Park Hyatt Zanzibar.

Akizungumza kuhusu tamasha hilo, Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rashid Juma alisema tamasha hilo zuri kwa watalii na wazawa kupata nafasi ya kula vyakula vya mataifa mengine ambavyo vitakuwa vikipatikana katika tamasha hilo.

Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rashid Juma akizungumza kuhusu Tamasha la Chakula la Mji Mkongwe.

“Tamasha hili lilianza mwaka jana kwa mafanikio makubwa na lilikuwa wazo ambalo lingesaidia sana kuleta watalii, migahawa 20 ilishiriki na wananchi waliitikia wito kama sehemu ya utalii wa ndani, lengo kubwa ni kukutanisha hoteli mbalimbali katika mji mkongwe visiwani Zanzibar,

“Matarajio ya mwaka huu hoteli kubwa na maigahawa zaidi ya 25 tunatarajia inatashiriki, kwasasa tumeshapokea maombi 26 za wanaotaka kushiriki lakini pia tumeweka kiwango kuwa itakuwa 35 na haitazidi hapo,” alisema Waziri Juma na kuongeza.

“Kuna wageni mbalimbali watakuja kutoka mataifa kama Mexico, Italy, nchi za Ulaya, Uingereza, Ujerumani, nchi za Asia, China na nchi mbalimbali na hawa wote wanataraji kupata chakula cha kwao na kinachopikwa Zanzibar. Kutakuwa na wapishi mashuhuri wengine watatoka Park Hyatt ya Zanzibar.”

Aidha Waziri Juma alisema serikali itashirikiana na waandaji tangu mwanzo hadi mwisho ili kufanikisha tamasha hilo na kuwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na wasihofie bei ya chakula kuwa juu kwani wamepanga kuhakikisha kuwa bei ya chakula inakuwa ya kawaida ili kila mwananchi aweze kushiriki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Park Hyatt Zanzibar na Hyatt Regency Dar es Salaam, Garry Friend akizungumza kuhusu Tamasha la Chakula la Mji Mkongwe.

Share:

Leave a reply