Tamasha la Sauti za Busara 2017 kuanza rasmi jioni ya leo, Vikundi 9 kuwasha moto

522
0
Share:

MO  BLOG-ZANZIBAR: Tamasha la Sauti za Busara kwa msimu wa 14, limeanza rasmi mchana wa leo kwa kuanza na Paredi iliyokusanya vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ambao kwa pamoja waliweza kutemba kutoka eneo la Kisonge mpaka viunga vya Ngome Kongwe mahala ambapo linnafanyika jukwaa kubwa la tamasha hilo.

Uongozi wa Busara Promotions wenye makao yake Visiwani Zanzibar,  kwa mujibu wa ratiba yao leo jumla ya vikundi 9, vinatarajia kuwasha moto katika tamasha hilo kubwa. Miongoni mwa vikundi hivyo ni pamoja na kundi la Batimvo Percussion Magique kutoka Burundi,  Pia watatumbuiza kundi la Loryzine (Reunion).

Swahili Encounters (Zanzibar/ Various), Grace Barbe (Shelisheli),  Rajab  Suleiman &Kithara (Zanzibar), Wahapahapa Band (Tanzania), Mswano Gogo Vibes (Tanzania), Sami Dan& Zewd Band (Ethiopia) na The Spirits Band (Tanzania).

Vikundi hivi vyote vitatoa burudani ya moja kwa moja ‘Live’ kwa kutumia vifaa vya muziki ala.

Tazama MO tv kuona matukio yote ya ufunguzi wa Sauti za Busara 2017:

Vikundi vya Paredi vikiwa katika maandamano hayo katika maeneo mbalimbali ya Ngome Kongwe Zanzibar.

Vikundi vya Vijana wakitoa burudani

Ulinzi asilimia 100 ndani ya tamasha la Sauti za Busara 2017

Bendi ikiongoza maandamano

Burudani zikiendelea

Vikundi vikiendelea kutoa burudani

MC wa shughuli upande wa burudani Mc Muslim Nassor Jazzfaa akiwa katika tukio hilo

burudani ya Ngongoti

Batimvo Percussion Magique kutoka Burundi ikitoa budani

Mbwembwe za Paredi

Mmoja wa Crew wa Sauti za Busara 2017 akifuatilia mambo katika tamasha hilo

Duka la bidhaa za zinazouzwa kutoka Sauti za Busara 

Bidhaa za nguo ambazo zinapatikana ndani ya tamasha hilo. Picha zote na Andrew Chale, MO BLOG-ZANZIBAR.

Share:

Leave a reply