Tambo za Haji S. Manara: “Afe kipa afe beki, watafungwa tu”

762
0
Share:

Mpira ni mchezo unaochezwa hadharani, hauchezewi chumbani, na mpira ni mchezo wa takwimu, hasa huu mpira wa kisasa, kuelekea feb 25 Simba anaongoza ligi na ameongoza kwa raundi nyingi ni zaid ya 90%ya mizunguko yote tuliocheza hadi sasa.

Achana na kuongoza ligi ,Simba ndio timu pekee hadi sasa iliyofuzu kwa robo fainali ya kombe la Shirikisho,wengine watafata tu.

Takwimu pia znatubeba, tumeongoza kwa kumiliki mpira katik michezo yote ya ligi kuu na kombe la shirikisho, kuliko timu yoyote hadi sasa, hata kwenye michezo iliyopoteza, Simba walikuwa bora katika umiliki wa mpira uwanjani, mbali ya timu iliyotengeneza nafasi nyingi za magoli kuliko timu yoyote ya ligi kuu msimu huu.

Ukiachana na hilo nani anabisha Simba ndio timu yenye ukuta mgumu kwenye  ligi kuu? tukiruhusu wavu wetu kutikiswa mara saba tu? sijui kama wajua pia, Simba haijawahi kufungwa mchezo wowote ule kwa tofauti ya goli moja, wenzetu hadi NNE washachezea!!

Najua wafahamu pia kwa sasa hakuna beki imara anayemfikia walau nusu Method Mwanjale!!sijui nini niseme kuhusu Ajibu, Mavugo na MO!!

wakitoka wakapige mnada lile jengo lao liliokuwa bondeni kule wanapofugia chura.

Nini Haji Manara anajivunia kuelekea feb 25?

Hiz ni takwimu na namba, wazungu wanasema ‘numbers dont lie’, namba haziongopi, tutawafunga, narudia tutawafunga, TUTAWAFUNGA bila wasiwasi.

Uzuri wake tupo vzuri ndani na nje ya uwanja,hatuna makando yoyote hata katika uongozi, tumetulia tuliii kama barafu, wenzetu ndio hvyo tena kama mlivyosikia!!

Kikubwa waamuzi waje kuchezesha kwa kufuata sheria 17, TFF wanajua na nchi inajua, tunataka mshindi halali, hatutaki kubebwa na hatutakubali kuonewa, huku pia tukiwataka washabiki wetu wawe watulivu, na tunaenda kujaza uwanja, kila mwana Simba na aje, avae jezi zetu na tununue mapema tiketi zetu kupitia Selcom.

Twendeni tukawadhalishe Taifa Februari 25.2017, twendeni mkamuone ‘King Loudie’, twendeni mkauone udambwi wa MO na Ajibu, twendeni mkazione Sambusa za mboga mboga pale Taifa, tutahanikiza mwanzo mwisho huku tukiwacharura wenzetu kwa mambo yao yaleeeeee…

Ahhh ntaandika daily kuelekea feb 25, leo mwanzo tu. Ijumaa njema

Haji Manara (Pichani juu)

Kikosi cha Simba Sc

 

Share:

Leave a reply