TANAPA na TBC yatiliana saini kuanzisha chaneli maalum ya Utalii nchini

373
0
Share:

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa pamoja leo wamesaini makubaliano ya kuanzishwa kwa Chaneli maalum ya Utalii itakayohusika na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dk. Ayub Rioba na Kaimu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu.

Wakuu hao wa mashirika wakitiliana saini mikataba hiyo mapema leo nchini

Wakuu hao wakionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani baada ya kumalizika kwa utilianaji wa saini mikataba hiyo mapema leo nchini.

Chanzo: Meneja Mawasiliano wa Tanapa,Pascal Shelutete

Share:

Leave a reply