Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Afrika wa Bima ya Maisha 2017

326
0
Share:

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa Semina ya Bima ya Maisha 2017 utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba, 1 – 3 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha.

Akizungumza kuhusu mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Khamis Suleiman amesema mkutano huo utajikita katika dhima ya kuangalia namna sekta ya bima inaweza kusaidia katika mapinduzi ya viwanda na maendeleo na tayari watu zaidi ya 150 wamethibitisha kushiriki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mkutano wa Afrika wa Bima ya Maisha, Khamis Suleiman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano habari.

“Kuna nchi zaidi ya 20 zitashiriki katika mkutano huu na mada zitakazozungumziwa ni pamoja na zile zitakazosaidia mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutakuwa na dama za bima kuangalia wapi tulipo na wapi tunapotaka kwenda,

“Azma yetu ni kuleta msisimko kwa wananchi husasi kwa wananchi kununua kiwango kikubwa cha bima kuliko ilivyo sasa hivi kwa kuongeza mteja mmoja mmoja na kuongeza mapato kwa taifa,” amesema Seleiman.

Aidha Suleimani amesema mkutano huo utatumika kusaidia kukuza sekta ya utalii, “Tumeona hii ni fursa ya kipekee kuendeleza soko letu la utalii na ndiyo maana tumeamua kufanya mkutano huu Arusha na kutakuwa na siku moja ya kuwapa fursa wajumbe kuweza kutembelea vituo vya utalii.”

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa Afrika wa Bima ya Maisha, Magreth Ikongo akizungumza na waandishi wa habari.

Naye mjumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, Magreth Ikongo amesema kutakuwa na watoa mada kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na hata nje ya Afrika lakini pia washiriki watapata nafasi ya kubadilishana uzoefu na hivyo kuyataka makampuni ya bima ya hapa nchini kutumia vyema mkutano huo wa siku tatu.

 

“Kutakuwa na watoa mada kutoka Afrika Kusini, Kenya na Geneva, Switzerland, mada zinalenga kushirikisha uzoefu na tunatarajia makampuni ya bima ya Tanzania kupata uzoefu kutoka kwa makampuni mengine na kuweza kuongeza kasi katika kuchochea maendeleo hususani katika viwanda ambapo ndiyo lengo la taifa,” alisema Ikongo.

Share:

Leave a reply