Tanzania yafanikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano – Ummy Mwalimu

190
0
Share:

Tanzania imekua miongoni mwa nchi chache katika bara la Afrika kufanikiwa kufikia lengo la nne la maendeleo ya millennia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Hayo yamesemwa na waziri wa afya,maendeleo ya jamii ,.jinsia,wazee na watoto  Ummy mwalimu  wakati akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaofanyika nchini Geneva,Uswisi.

Ummy alisema licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali Tanzania imepiga hatua  katika sekta ya afya kwa kupunguza vifo hivyo hadi kufikia  vifo 54 kati ya vizazi hai 1,000 kutoka vifo 112 kati ya vizazi hai 1,000.

Aidha, mkutano huo ambao ni wa ngazi ya juu katika sekta ya afya duniani, Tanzania imetambuliwa na kutangazwa kuwa miongoni mwa nchi zilizotokomezwa ugonjwa wa polio kwa kufanikiwa katika utoaji wa huduma za chanjo nchini kwa watoto.

Mh. Ummy Mwalimu, Geneva

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, akihutubia mkutano wa 69 wa afya duniani unaoendela nchini Geneva-Uswisi.

“Ninaeleza kwa masikitiko kuhusu tatizo la mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliopo nchini Tanzania  ambapo hadi kufikia  tarehe 22 Mei, 2016 idadi ya wagonjwa ilifikia 21,581,kati yao watu 338 wamepoteza maisha,naahidi Serikali kupitia wizara ya afya  itaimarisha  na kuzingatia kanuni za afya ya mazingira katika kukabiliana na ugonjwa huu”alisema

Kwa upande wa kutokomeza malaria waziri Ummy alisema Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu kutoka asilimia 18 hadi 9.5 kwa Tanzania bara na kwa upande wa Zanzibar  imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa  hadi kufikia asilimia 0.6 .

Katika kuboresha huduma za afya nchini alisema Serikali ya Tanzania imejipanga na kuhakikisha itaboresha huduma za afya ziweze kumfikia kila mtanzania  popote alipo, “ili kuweza kufikia malengo haya ni wakati muhimu sasa kuwekeza zaidi katika sekta hii kwa kuongeza uwekezaji katika raslimali fedha,watu pamoja na kuboresha miundombinu ikiwemo utoaji wa huduma za afya nchini”.

Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Tanzania bara Mhe.Ummy Mwalimu kushoto akiwa na Waziri wa Afya wa visiwani Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nyuma yao ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Tanzania bara Dkt. Mpoki Ulisubisya

Waziri Ummy alisema katika kufikia mafanikio ,wizara ya afya inatarajia kuwasilisha muswada wa sheria katika bunge la mwezi wa Septemba,2016 wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya kitu ambacho kitakuwa ni mkombozi mkubwa kwa mwananchi katika kupata huduma za matibabu wakati wowote anapokuwa na fedha  au kutokuwa na fedha kwa kuwa maradhi hayachagui wakati.

Mkutano mkuu wa mwaka  wa Afya Duniani hufanyika  nchini Geneva –Uswis kila mwaka mwezi mei ambao huwakutanisha  mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa  Shirika la afya Duniani {WHO} na kuhudhuriwa na wadau,mashirika na taasisi zinazoshiriki katika kutoa huduma za afya Duniani.Tanzania inawakilishwa na waziri wa afya Tanzania bara Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo.

Waziri Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Kombo wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye mkutano huo unaowakutanisha mawaziri wa afya kutoka nchi wanachama wa shirika la afya duniani(WHO), nyuma yao ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Tanzania bara Dkt. Mpoki Ulisubisya

Share:

Leave a reply