Tanzania yaishangaza Iran kwa kutokua na dini

536
0
Share:

Meya wa Jiji la  Dar es salaam Isaya Mwita amekuwa gumzo katika mkutano uliomalizika jana Jijini Mashahad Nchini Iran baada ya kusema kwamba Tanzania haina dini ila watu wake wana dini.

Mwita ambaye yupo Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku 10, alijikuta kwenye gumzo hilo wakati akichangia mada iliyokuwa ikiendelea ndani ya mkutano huo ambao ulimalizika jana.

Alisema kwamba Tanzania ni Nchi ya amani ambayo haijawahi kuwa na ubaguzi wa rangi, dini wala kabila na kwamba kila mmoja aliyepo ndani ya nchi hiyo  anajivunia kuwa mtanzania.

“Watanzania kuna mambo ambayo tulijiwekea tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo ndio msingi mkuu tulionao, hakuna ubaguzi wa dini wala rangi, jambo kama hili ni maeneo machache sana katika Nchi zetu kuyakuta,hivyo Tanzania tunajivunia kuwa na utamaduni huu,” alisema Meya Mwita.

Alisema hali hiyo imekuwa ni tofauti hata katika maeneo mengine kwani yapo mataifa ambayo hadi sasa yanajadili udini na ukabila , na kushauri kwamba ni vema viongozi wa kila majiji kujitahidi kutumia nafasi hiyo ili kuondokana na matabaka.

Alieleza kwamba “Jumuiya za kimataifa zimekuwa zikiwatazama waislam wote  kama watu ambao si  salama nakushauri kwamba haki za kibinadamu zizingatiwe kwao kwakuwa wote tunaombwa na Mungu mmoja” 

Aliongeza kwamba “Wapo watu ambao wanaitumia dini ya kiisilamu  vibaya, nakuchafua watu wengine , lakini tunatakiwa kutambua kwamba kila wote hapa tumeumbwa na Mungu mmoja, sasa dini zetu zisitufanye tukashindwa kushirikiana na kuzungumza lugha moja”

Baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Mwita kesho ataelekea jijini Tairan kwa mualiko wa Meya wa jiji hilo ambapo pamoja na mambo mengine huko atatembelea ofisi za umma na kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya kujadili namna ya kuendesha majiji sambamba na kutatua changamoto.

 

Share:

Leave a reply