Tanzania yapanda nafasi 13 katika viwango vya FIFA

269
0
Share:

Kama ilivyo kawaida ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kutoa orodha ya viwango vya nchi zinazoongoza katika mchezo wa soka kwa kila mwezi, imetoa orodha ya mwezi Juni, viwango ambavyo vimeipandisha Tanzania kwa nafasi 13.

Viwango hivyo ambavyo vimewekwa katika mtandao wa Fifa, Tanzania imeonekana kupanda hadi nafasi ya 123 ikitokea nafasi ya 136 iliyokuwa nayo awali.

Tanzania imepanda nafasi hiyo ikiwa haijacheza mchezo wowote tangu ilipocheza na timu ya taifa ya Misri katika uwanja wa taifa Dar es Salaam na Tanzania kupokea kipigo.

Kwa upande wa Afrika, Tanzania inashika nafasi ya 33.

Kwa dunia, Argentina inashika nafasi ya kwanza, kwa Afrika nchi ya Algeria inaongoza na kwa Afrika Mashariki, Uganda inashika nafasi ya kwanza.

Share:

Leave a reply