Tanzania,Zambia zasaini makubaliano ya kuanzisha kituo cha pamoja cha Forodha

404
0
Share:

Tanzania n Zambia, zimetiliana saini Mikataba Minne kwa ajili ya uanzishwaji  rasmi wa kituo cha pamoja katika mpaka wa Tunduma na Nakonde,  kitakachoanza kufanyakazi rasmi Februari mosi mwaka huu, ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili

Uamuzi wa  kuanzishwa kwa huduma hiyo ijulikanayo kama One Stop Border Post, ni utekelezaji wa maagizo ya Marais wa nchi hizo Mbili, Waheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, na Edger Lungu, waliyoyatoa wakati Rais huyo wa  Jamhuri ya Zambia, Edger Lungu alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini hivi karibuni.

Mikataba iliyotiwa saini ni makubaliano ya  Mwongozo wa Utendaji wa Kituo cha Pamoja cha Tunduma/Nakonde pamoja na  Mfumo wa Urahisishaji Biashara kwa lengo la kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

Waliosaini Mikataba hiyo kwaniaba ya Serikali ya Tanzania, Mjini Vwawa, wilaya ya Momba, mkoani Songwe, ni Naibu Katibu  Mkuu wa Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, huku Zambia  ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa nchi  hiyo, Bi. Kayula Siame.

Wakizungumza baada ya kutiwa saini  kwa mikataba hiyo Makatibu wakuu hao wamesema kuwa Uanzishwaji wa Kituo  cha Pamoja Mpakani Tunduma/Nakonde, utarahisisha ufanyaji wa biashara  kati ya Tanzania na Zambia kwa kupunguza ukaguzi kwani ukaguzi  utafanyika mara moja katika kituo cha kuingia badala ya kufanyika mara  mbili katika nchi zote mbili pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi

“Lengo la kituo hicho pia ni kuifanya biashara kati ya Tanzania na Zambia kuwa huru lakini ikifuata misingi na taratibu za kufanya biashara mpakani.

Pia kitarahisisha biashara katika eneo la mpakani na kuvutia wananchi na wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kutumia kituo hiki na kuepuka  kutumia njia zisizo rasmi kupitisha mizigo na hivyo kupunguza ufanyaji  wa biashara za magendo kama si kukomeshwa kabisa” Alisisitiza Bi. Amina Khamis Shaaban

Alisema kuwa utaratibu huo unatarajia kuona  kuongezeka kwa ushirikiano kati ya taasisi za serikali za nchi hizi  kwani shughuli katika kituo zitakuwa zinafanyika kwa uwazi katika eneo  moja.

Benny Mwaipaja-WFM, Mbeya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini mmoja wa Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo hicho ifikapo Februari Mosi, 2017.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini moja ya mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza kufanyakazi rasmi Februari mosi, 2017.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja cha Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.

Share:

Leave a reply