TBL Group yachangia ongezeko la mauzo ya DSE kwa asimilia 99

236
0
Share:

Idadi ya mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeongezeka kwa asilimia 39% na kufikia Tsh. 5.3 Bilioni kutoka 3.8 Bilioni, wakati idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 91% hadi 869,453 kutoka 9.8 Milioni wiki iliyopita, kuisha Ijumaa ya tarehe 31 Oktoba 2016:

Meneja wa Miradi na Masoko DSE, Patrick Mususa leo Septemba 31, 2016 amewaambia waandishi wa habari kuwa, kampuni ya bia ya TBL imechangia ongezeko la idadi ya mauzo kwa asilimia 99 kutokana na kaunta zake kupunguza bei ya hisa.

Mususa amesema ukubwa wa mtaji wa soko hilo umepanda kwa asilimia 1% na kufika Trilioni 21.8 kutoka Trilioni 21.6 wiki iliyopita. Huku Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.4% hadi Trilioni 8.19 kutoka Trilioni 8.16 wiki iliyopita.

Hata hivyo, Mususa amezitaja kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kuwa ni CRDB kwa 51.8%, TBL kwa asilimia 44.44% na DCB kwa 1.22%.

Amesema Viashiria katika Sekta ya viwanda vimeongezeka zaidi ya pointi 26 baada ya bei ya hisa za TBL kuongezeka kwa asilimia 0.76%:

Amesema, bei za hisa za makampuni mengine ya ndani ziliendelea kubaki kwenye kiwango kile kile na kupelekea viashiria vya sekta za huduma za kibenki na za kibiashara kubakia kwenye kiwango kile kile wiki hadi wiki.

Share:

Leave a reply