TCRA yazipiga faini kampuni za simu kwa kutofuata taratibu za usajili wa laini

471
0
Share:

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini ya Sh bilioni 11 kampuni sita za simu kwa kutofuata taratibu za usajili wa laini za simu.

Kampuni ambazo zimepigwa faini ni Halotel imetozwa Sh bilioni 1.6, Smart Sh bilioni 1.3, Airtel Sh bilioni 1.08, Vodacom Sh milioni 945 na Zantel Sh milioni 105.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba amesema, kampuni kampuni hizo zimepigwa faini kutokana na kusajili laini mpya bila kutumia vitambulisho vinavyotakiwa.

Share:

Leave a reply