TFF yamfungulia mashtaka ya kinidhamu Haji Manara

885
0
Share:
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefungulia mashtaka ya kinidhamu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kwa Kamati ya Maadili kwa madai ya kutumia maneno ambayo yanayoonekana kutokuwa na maadili na taratibu za soka.
·      
TFF imetoa taarifa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, zaidi waweza kusoma hapa chini; Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.

Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali.
Ili kutunza heshima ya mpira wa miguu Tanzania, wanafamilia wa mchezo huo
katika kutimiza masharti ya kanuni za maadili za TFF, hawana budi kuheshimu na
kufuata taratibu zote hizo ndani na nje ya uwanja.
Taswira njema ya shirikisho inajenga imani ya wadau wakiwamo serikali,
mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, vyombo vya habari, vyama vya mpira vya
kimataifa, NGO’s na watu binafsi kwa taasisi (TFF). Kinyume chake ni kulibomoa
shirikisho.
Dhima ya uongozi wa TFF ni pamoja na kulinda na kutunza heshima hii. Hivyo
vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjaji wa maadili havitavumiliwa, na
vikitokea hatua zitachukulia.
Na kwa muktadha huu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, limemfungulia
mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya
nidhamu. Leo hii Aprili 21, 2017 atapewa mashtaka yake na kujulishwa lini na
wapi yatasikilizwa.
TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao
kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza
heshima ya mpira wetu.

Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali. Wanafamilia wa mpira wa miguu ni pamoja na wachezaji, makocha, waamuzi, viongozi wa mpira wa ngazi zote na waajiriwa wa taasisi ambazo ni wanachama wa TFF wa ngazi mbalimbali. Ili kutunza heshima ya mpira wa miguu Tanzania, wanafamilia wa mchezo huo katika kutimiza masharti ya kanuni za maadili za TFF, hawana budi kuheshimu na kufuata taratibu zote hizo ndani na nje ya uwanja. Taswira njema ya shirikisho inajenga imani ya wadau wakiwamo serikali, mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, vyombo vya habari, vyama vya mpira vya kimataifa, NGO’s na watu binafsi kwa taasisi (TFF). Kinyume chake ni kulibomoa shirikisho. Dhima ya uongozi wa TFF ni pamoja na kulinda na kutunza heshima hii. Hivyo vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjaji wa maadili havitavumiliwa, na vikitokea hatua zitachukulia. Na kwa muktadha huu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya nidhamu. Leo hii Aprili 21, 2017 atapewa mashtaka yake na kujulishwa lini na wapi yatasikilizwa. TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza heshima ya mpira wetu.

A post shared by Tanzania Football Federation (@tanfootball) on

Share:

Leave a reply