TFF: ”Yanga wanaweza kusamehewa usajili FIFA endapo watalipa Dola 500 kwa kila mchezaji”

258
0
Share:

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeeleza kuwa, Klabu ya Yanga inaweza kupata nafasi ya kusajili wachezaji wake katika mfumo wa  Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA),endapo watalipa gharama ya kiasi cha Dola 500 kwa kila mchezaji mmoja.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Agosti 12.2016 Afisa Habari na Mawasiliano, Bwana Alfred Lucas amebainisha kuwa, suala la Yanga wao kama Chama cha Soka wameshughulika nao na tayari kuna uwezekano wa FIFA kutoa adhabu ilikuweza kuwaruhusu Yanga kufanya usajili wao.

“Kuna uwezekano mkubwa kwa Yanga kupata nafasi ya kufanya usajili wao FIFA, kwani tayari tumeshapelekea utetezi wao na tunasubiria maamuzi. Ila kwa taratibu za FIFA inataka kila mchezaji mmoja analipa kiasi cha dola za Kimarekani 500 (USD 500) huku kwa klabu za Ligi ya daraja la Kwanza  na Pili wakitakiwa kulipa kiasi cha Dola 250.” Alieleza Msemaji huyo wa TFF.

Hadi sasa ni kalabu za Yanga na Coastal Union ya jijini Tanga ndizo timu zilizoshindwa kuwasilisha kwa muda majina hayo ambapo licha ya kuwasilisha utetezi wao bado FIFA wanafanyia kazi.

“Kwa kawaida usajili huo lazima uingizwe kwenye Mtandao wa Usajili wa Kimataifa (TMS) ambao huwa kumbukumbu hizo hutunzwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), na wakati Yanga wao wanashughulikia suala hilo, kulikuwa na tatizo kubwa la kimtandao yaani mawasiliano ya Intaneti yalikuwa yapo chini sana hivyo walishindwa kujaza kwa wakati” alieleza Msemaji huyo wa TFF juu ya utetezi  walio utoa Yanga kwenda FIFA.

Hata hivyo kwa  mujibu wa kanuni za FIFA, klabu inayochelewesha kutuma majina ya wachezaji itakaowatumia inatakiwa kutoa utetezi unaojitosheleza na endapo ukikataliwa timu husika hushuka daraja ambalo halimo kwenye usajili wa mfumo wa TMS.

Kwa mujibu wa Msemaji huyo wa TFF, Alfred Lucas amebainisha kuwa, Klabu hiyo ya Yanga ina wachezaji zaidi ya 24 hivyo endapo itawafanyia usajili huo wa mfumo wa TMS, ambapo kwa kila mchezaji mmoja anagharamia Dolla 500 (USD 500)

 kwa kiwango cha kubadilisha fedha kwa Tanzania ambapo mchezaji mmoja pekee atagharimu zaidi ya Milioni moja (Mil.1) hii pia itategemea kupanda na kushuka kwa Dola katika soko la kubadilishia fedha za kigeni, hivyo kwa wachezaji wote 24 Yanga wanaweza kutumia zaidi ya Milioni 30.

Tazama MO tv:

Fifa-TMSKamati za FIFA zinazopitia TMS za wachezaji wote Duniani wakiwa katika moja ya kikao chao hicho

DSC_5315Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Bwana Alfred Lucas akizungumzia suala la Yanga na hatua ya FIFA kuhusiana na usajili kupitia mfumo TMS ambao hadi sasa Wanajangwani hao tayari wameuchelewa. (Picha na Andrew Chale)

Share:

Leave a reply