Timu za Panama Iringa,Marsh Academy kucheza leo katika Ligi ya Wanawake

283
0
Share:

Raundi ya Pili ya Duru la Kwanza ya Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake inaendelea tena leo  Novemba 8.2016  kwa mchezo mmoja  utakaowakutanisha  Panama ya Iringa ambao watakuwa wageni wa timu ya Marsh Academy kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Lakini, wakati mchezo huo Na. 5 wa Kundi B, ukifanyika michezo mingine mitano ya raundi ya pili ikiwamo mitatu ya Kundi A, imebidi iahirishwe na itapangiwa tarehe nyingine. Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa michezo hiyo ni uwingi wa wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Wanawake – Twiga Stars.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, michezo ya Kundi B iliyoahirishwa ni kati ya Majengo Women ya Singida iliyokuwa icheza na Baobab ya Dodoma kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mechi nyingine ni kati ya Victoria Queens ya Kegera iliyokuwa icheze na Sisters ya Kigoma – mchezo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Katiba mjini Bukoba.

Michezo ya Kundi A iliyoahirishwa ni kati ya Fair Play ya Tanga iliyokuwa iikaribishe Mburahati Queens ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilihali michezo mingine iliyoahirishwa ni ya Novemba 9, ambako JKT Queens ya Dar es Salaam ilikuwa icheze na Viva Queens kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Evergreen Queens na Mlandizi zilikuwa zitumie Uwanja wa Karume, Ilala kucheza mechi yao hiyo.

Share:

Leave a reply