TIRA yazindua waraka kuhusu masharti ya kufanya biashara na makampuni ya nje ya nchi

283
0
Share:

Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), imezindua waraka Na. 055/2017 ambao unahusu masharti ya kufanya biashara na makampuni ya bima mtawanyo na madalali wa bima mtawanyo kutoka nje ya nchi ambao utaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2018.

Akuzungumza na waandishi wa habari kuhusu waraka huo, Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware alisema waraka huo ni sehemu ya jitihada za serikali kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kutokana na kupeleka biashara za bime nje ya nchi kupitia utaratibu ujulikanao kama mtawanyo.

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waraka Na. 055/2017.

“Naomba itambulike kuwa utaratibu wa kupeleka biashara za bima nje ya nchi ni suala la kawaida katika masoko ya bima duniani, hivyo utaratibu huu unapofanyika vizuri huleta faida anuai kwa soko la ndani kama kushirikiana na makampuni ya bima ya nje katika kulipa hasara zitokanazo na majanga ya ndani ya nchi,

“Kuimarisha mapato na mitaji ya makampuni ya bima ya ndani, usimamizi mzuri wa madai, kuimarisha uwezi wa kitaalam na watendaji katika sekta ya bima nchini na kulinda mitaji ya makampuni ya bima nchini,” alisema Dkt. Saqware.

Kamishna wa Bima nchini, Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari kuhusu waraka Na. 055/2017.

Dkt. Saqware alisema mamlaka imetoa waraka huo ili kudhibiti mwenendo hasi na kuimarisha ufanisi katika upelekaji wa biashara za bima mtawanyo nje ya soko la bima la hapa nchini.

“Ni matarajio waraka huu utasaidia kuimarisha kiwango cha tozo za bima zinazobakizwa hapa nchini hivyo kuongeza kiwango cha mchango wa sekta ya bima katika rasilimali fedha na uchumi wa ndani, kuyapa makampuni yote bima nchini fursa ya kuimarisha mapato yao,” alisema Dkt. Saqware.

Share:

Leave a reply