Leicester, Tottenham zaongoza kwa kuingiza wachezaji wengi katika Kikosi Bora cha Mwaka EPL

277
0
Share:

Orodha ya wachezaji 11 waliopo katika Kikosi Bora cha Mwaka cha Ligi Kuu ya Uingereza kimetangazwa ambapo Vinara wa Ligi hiyo, Leicester City na timu inayoshika nafasi ya pili, Tottenham wakiibuka vinara kwa kutoa wachezaji wanne kila timu.

Wachezaji wa Leicester City walioingia katika kikosi hicho ni Jamie Vardy, Riyad Mahrez, N’Golo Kante na Wes Morgan huku Tottenham wakiwa na Harry Kane, Dele Alli, Toby Alderweireld na Danny Rose.

Vilabu vingine vilivyopata nafasi ya kuingiza wachezaji ni Manchester United kupitia David De Gea, Arsenal kupitia Hector Bellerin na West Ham kupitia Dimitri Payet.

Share:

Leave a reply